Transfer Multisort Elektronik ni kampuni ya kifamilia iliyoanzishwa mnamo mwaka 1990. Hapo mwanzoni, ilikuwa ni duka dogo la kuuza vifaa vya kielektroniki kwa vituo vitoavyo huduma za kielektroniki na watengenezaji wadogo wadogo.
Kwa sasa, TME inaongoza katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki, vifaa vya karakana na vifaa vingine vya kiautomatiki vinavyotumika katika uendeshaji wa mitambo viwandani barani Ulaya.
Twauza zaidi ya bidhaa 250,000 zilizotengenezwa na watengenezaji mashuhuri wa vifaa vya kielektroniki vilivyo na ubora wa hali ya juu. Nyingi za bidhaa hizi zapatikana katika bohari letu.
Kwa zaidi ya miaka 28, tumekuwa tukiwahudumia wateja kupitia:
Mwaka 2016, imeanzishwa idara mpya maalumu kwa ajili ya kuhudumia wateja wetu kutoka Afrika pamoja na Mashariki ya Kati. Wataalamu wetu wanazungumza lugha mabalimbali zikiwemo: Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, na Kiswahili.
Lengo letu ni kutoa huduma bora kwa wateja wetu kutoka Afrika na pia Mashariki ya Kati kwa mahitaji yao ya vifaa vya kielektroniki kwa bei nafuu na kuwasilisha kwa muda mfupi iwezekanvyo. Zaidi ya hayo, twajitahidi kukuza elimu kwenye sekta ya kielektroniki kwa kushirikiana na sekta mbali mbali zinazojihusisha na mafunzo ya kisayansi na teknolojia.
Sasa, tunahudumia wateja 200,000 wa B2B na B2C katika nchi 140. Tunamiliki kampuni 10 katika Ulaya (katika Ucheki, Hungaria, Slovakia, Ujerumani, Romania, Hispania, Italia, Uholanzi, Ufalme wa Maungano na Uchina).
Tunauza katika masoko ya Afrika, Mashariki ya Kati, Uchina na Amerika.
Katika uuzaji wetu, kuna zaidi ya bidhaa 250,000 zilizotengenezwa na watengenezaji mashuhuri wa vifaa vya kielektroniki na kiautomatika. Watengenezaji wote wanatimiza kanuni na viwango vya ubora wa hali ya juu wa vifaa vyote vizalishwavyo barani Ulaya.
Mwanzoni mwa mwaka wa 2017, wateja wetu kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wataweza kununua vifaa vya kielektroniki, vifaa vya karakana, vifaa vya kiautomatiki na vifaa vingine viwezeshavyo uendeshaji wa mitambo viwandani moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.tme24.com.
Duka letu jipya la mtandaoni litapatikana kwa lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kiswahili, na Kituruki. Kwa sasa, katika tovuti yetu ya www.tme.eu kuna toleo la Kiingereza la duka letu la mtandaoni ambapo unaweza kununua kila kitu unachohitaji kwa mahitaji yako yote ya kielektroniki.
Ikiwa unahitaji kuwasiliana nasi, tuandikie barua pepe moja kwa moja kupitia anwani zifuatazo:
mena@tme24.com (Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati)
africa@tme24.com (Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara)
Kuna mbinu tatu za kuagiza:
Uhawili wa pesa wa kielektroniki na malipo kwa kutumia kadi za malipo yanatekelezwa kupitia PayPal.
Usafirishaji wa Anga wa bidhaa za hatari kama (mabomu, vifaa viwakavyo, gesi, n.k) haviungwi mkono na DHL Express pamoja na UPS Express Saver.
TME Education ilianzishwa na Transfer Multisort Elektronik mnamo mwaka 2016. Lengo letu ni kuwashughulikisha vijana kutoka pande zote za dunia kubadilisha uhalisi wa jamii yao na kutengeneza nafasi bora kwao wenyewe kwa kurahihisha upatikanaji wa elimu ya elektroniki na msaada wa teknolojia. Zifuatazo ni harakati za mradi wetu wa elimu:
Tambua zaidi kuhusu TME Education na temebelea mtandao wetu.
Kama una maswali yoyote kuhusu mradi huu au unataka kushirikiana nasi, tuandikie kwa: contact@tmeeducation.com.
Ikiwa una maswali yoyote, tuandikie barua pepe kupitia mena@tme24.com au africa@tme24.com. Unaweza pia kutumia fomu ya mawasiliano iliyo hapa chini. Sehemu zenye alama ya kinyota (*) zinahitajika.
TME Africa & Middle East Office
33A Łagiewnicka Street
30-417 Kraków, Poland, Europe
Makao makuu ya TME - Maelezo ya mawasiliano
Transfer Multisort Elektronik Sp. z.o.o.
ul. Ustronna 41, 93-350 Łódź, Poland
tel. +48 42 293 52 99